Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.

  • 10 minutes 3 seconds
    Lugha ya kiswahili katika kuimarisha uelewa, uhamasishaji na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

    Wakati viongozi wa dunia, wanasayansi na watunga sera wanapokutana katika miji mikuu ya Dunia kujenga hoja kuhusu hatima ya sayari kupitia mikutano ya tabianchi ya Umoja wa Mataifa,  Wataalamu wa lugha,,  walimu pamoja na  wanafunzi waaendeleza  mijadala. Kaulimbiu ukiwa ni namna lugha adimu ya kiswahili inavyotumika katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

    19 December 2025, 5:53 am
  • 10 minutes
    Kituo cha jambo Redio nchini DRC chapokea tuzo kwenye COP30

    Nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kituo cha Jambo redio, kimejitwika jukumu la kuelimisha jamii kuhusu masuala ya mazingira na tabianchi, lakini muhimu sana ni haki zao.

    Katika mkutano wa tabianchi uliotamatika jijini Belem nchini Brazil, kituo cha Jambo Redio kilipokea tuzo kutoka kwa shirikika linalotetea haki za wanawake Women Engage for a Common Future, WECF. Kituo hiki, kimekuwa kikitoa habari kwa jamii ambazo wakati mwingine hazina uwezo wa kupata habari.

    15 December 2025, 11:22 am
  • 9 minutes 59 seconds
    COP30 uliotamatika jijini Belem, Brazil,, suala la ufadhili wa tabianchi, nishati safi ni miongoni mwa ajenda

     

    Miongoni mwa mambo yalioamuliwa ni kuhamasisha kiasi cha fedha trilioni 1.3 kila mwaka kufikia 2035 wa ajili ya hatua za tabianchi, kuimarisha fedha uhimilivu mara tatu kufikia 2035.

    Msikilizaji, suala la kuharakisha ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi inasalia kuwa kipaumbele  cha dharura hasa kwa nchi zinazoendelea ambazo zina athirika pakubwa na janga hilo.

    5 December 2025, 3:09 pm
  • 9 minutes 57 seconds
    Shirika la Weather Mtaani labuni teknolojia ya kuepuka majanga ya hali ya hewa Kibera

    Mvua huja kwa sauti ya baraka lakini katika kitongoji, sauti hiyo hubeba hofu. Maji yanapoteremka kutoka angani, katika sekunde chache, barabara hugeuka mito. Vyumba vya kulala vinageuka mabwawa. Katika kitongoji cha Kibera jijini Nairobi nchini Kenya, hali hiyo ya hofu imebadilishwa kupitia kundi la vijana linalojiita Weather Mtaani.

    Shirika la Weather Mtaani linatumia teknolojia ya simu kutafsiri jumbe za utabiri wa hali ya hewa kutoka kwa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa ya Kenya, kwa lugha inayoeleweka. 

    18 November 2025, 3:14 pm
  • 9 minutes 57 seconds
    Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi COP30 jijini Belem, Brazil

    Mkutano huu unakwenda kufanyika wakati ripoti mpya ya shirika la mazingira la umoja wa mataifa UNEP, ikionesha kuwa bado dunia iko nyuma katika kuafikia malengo ya mkataba wa Paris wa kudhibiti wastani wa jotoridi duniani kufikia nyuzijoto 1.5.

    12 November 2025, 1:23 am
  • 9 minutes 58 seconds
    Ripoti: Matajiri wachache wanateka nyara dunia kwa kuchangia pakubwa utoaji wa hewa ukaa

    Dunia inapojiandaa kwa mkutano wa kimataifa wa Mazingira COP30 utakaofanyika Belém, Brazil, ripoti mpya imeibua mjadala mkali—si tu kuhusu uzalishaji wa hewa ukaa, bali pia kuhusu ukosefu wa usawa.

    Utafiti mpya wa shirika la Oxfam, unaonesha kuwa mataifa tajiri na watu wachache wenye utajiri mkubwa wanachangia kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi.

    Inaitwa “ukosefu wa haki wa hali ya hewa.” Mtaalam wetu leo kulichambua hili ni David Abudho, anayeshughulika na mabadiliko ya tabia nchi barani Afrika kutoka shirika la Oxfam.

    6 November 2025, 11:41 am
  • 10 minutes 1 second
    Siku ya Chakula duniani: Mapendo Banque Alimentaire yapambana na ukosefu wa usalama wa chakula
    24 October 2025, 10:09 am
  • 9 minutes 50 seconds
    maadhimisho ya siku ya kimataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga

    Ripoti ya 2025 ya tathmini ya kidunia juu ya kupunguza hatari za majanga inakadiria kuwa gharama kamili ya kukabili majanga ni karibu dola trilioni2.3, na licha ya uwekezaji huu, bajeti za kitaifa bado ni za kiwango cha chini mno.

    18 October 2025, 8:26 am
  • 10 minutes
    Vijana walioasi uhalifu na kujitosa katika kutunza mazingira ya kijiji chao

    Fahamu kundi la vijana kutoka mtaa wa korogocho jijini Nairobi, walioasi uhalifu na kuamua kutunza mazingira ya jamii yao. Vijana hawa wananuia kuwa mfano kwa kizazi kijacho kufahamu kuwa hata juhudi ndogo zinaweza kuleta mabadiliko katika jamii inayowazunguka.

    7 October 2025, 7:55 am
  • 9 minutes 59 seconds
    Siku ya kimataifa ya hamasisho kuhusu upotevu na uharibifu wa chakula

    Wakati mamilioni ya watu wanalala njaa kila siku, chakula kizuri hutupwa mashambani, katika maduka makubwa, mikahawa - na ndiyo, hata katika nyumba zetu wenyewe.

    Uharibifu wa chakula sio tu kuhusu kile kilicho kwenye sahani zetu. Pia inahusu rasilimali zinazotumiwa kuzalisha chakula hicho: maji, ardhi, nishati, na raslimali watu, zote hupotea wakati chakula kinaharibika.

    29 September 2025, 4:20 pm
  • 10 minutes
    ACS2: Addis Ababa: Vijana wasisitiza uwekezaji kwenye ajira za kijani

    Uchumi wa kijani ni miongoni mwa mada kuu zilizojadiliwa kwenye mkutano wa pili wa mazingira wa bara la Afrika uliofanyika hivi majuzi jijini Addis ababa, ambapo wajumbe walijadili mikakati ya kufadhili maendeleo ya kijani barani Afrika kupitia masuluhisho yanayotegemea asili, teknolojia safi.

    Mjadala umeibuka kuhusu nafasi ya vijana katika mipango ya serikali za Afrika kuelekea uchumi wa kijani, kupitia ajira za kijani.

    29 September 2025, 12:26 pm
  • More Episodes? Get the App