• 10 minutes 5 seconds
    Maisha mapya: Jinsi akina mama vijana wanavyobadilisha ujuzi kuwa fursa

    Nchini Kenya, suala la mimba za utotoni ni changamoto. Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu ya taofa nchini Kenya kupitia utafiti wa mwaka 2022 asilimia 15 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 walikuwa wamewahi kupata ujauzito.

    Katika makala ya Gurudumu la Uchumi wiki hii, tunaangazia namna akina mama hawa wanavyogeuza ujuzi, juhudi na fursa za kiuchumi kuwa njia ya kujitegemea na kuwajengea watoto wao maisha yenye matumaini zaidi.

    9 September 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 4 seconds
    Umeme unaweza kuwa injini ya ukuaji wa uchumi Afrika Mashariki?

    Wikendi iliyopita, Tanzania ilizundua rasmi Mradi wa Umeme wa Maji wa bwawa la Julius Nyerere, lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huu, uliogharimu takribani shilingi trilioni 7.45 za Tanzania sawa na karibu dola za Marekani bilioni 2.9, unaongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa Tanzania kuzalisha umeme.

    Katika Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunajiuluza Je, megawati hizi zitageuka kuwa uzalishaji, ajira, biashara na ukuaji wa uchumi?

    26 August 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 3 seconds
    Goma: Wanawake wapambana na umaskini licha ya changamoto za usalama.

    Msikilizaji katika mazingira ambayo migogoro na changamoto za kiuchumi zimeathiri maisha ya kila siku ya wananchi, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta njia mbadala za kujipatia kipato na kuendesha familia zao.Hali hii inashuhudiwa katika mji wa Goma, mashariki mwa DRC, ambako baadhi ya wanawake wamegeukia ufugaji wa kuku kama njia ya kujikimu, hasa baada ya shughuli za baadhi ya taasisi za kifedha kutatizika katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi wa AFC-M23.

    19 August 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 1 second
    Je, Nchi Inaweza Kuendelea Bila Dira ya Maendeleo?

    Msikilizaji taifa linaweza kuishi siku moja baada ya nyingine bila kujua linaelekea wapi. Lakini taifa linalotaka kujenga uchumi imara, ajira bora na maisha bora kwa wananchi wake, linahitaji zaidi ya mipango ya leo, kwa kifupî linahitaji dira.

    Kwenye makala ya wiki hii tunaangazia dira ya taifa ni nini.

    12 August 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 3 seconds
    Sehemu ya Pili: Hatifungani ni nini na kwanini inakuhusu

    Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji.

    Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

    5 August 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 1 second
    Hatifungani za serikali na hazina: Kwa nini zinahusu kila mwananchi?

    Mara kadhaa tumesikia serikali zetu zikitangaza kuwa zinauza hati fungani za Serikali za muda mfupi na muda mrefu, yaani Government Bonds na Treasury bill, serikali zikikusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wawekezaji.

    Sasa je, hatifungani ni nini? Je, mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza?

    29 July 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 3 seconds
    Migogoro ya kimataifa inavyoathiri uchumi wa wananchi Afrika

    Katika Makala haya hivi leo tunajadili uhusiano kati ya siasa za kimataifa na uchumi wa wananchi wa Afrika, mara yingi tunasikia taarifa za vita, migogoro ya kisiasa au mivutano kati ya mataifa makubwa kama Urusi na Ukraine, Mashariki ya Kati, au migogoro inayovuruga usafirishaji wa bidhaa duniani. Kuzungumzia hili, hivi leo nimemualika Safari Fungo, mtaalamu wa masuala ya uchumi, utangamano wa kikanda na biashara za kimataifa akiwa Dar es Salaam, Tanzania.

    22 July 2026, 3:30 pm
  • 9 minutes 41 seconds
    Sarafu za kidijitali ‘Cryptocurrency’ uwekezaji wa kisasa wenye fursa na hatari

    Katika miaka ya hivi karibuni, sarafu za kidijitali maarufu kama cryptocurrency zimezidi kuvutia watu wengi duniani. Wapo waliopata faida kubwa, lakini pia wapo waliopoteza fedha nyingi kutokana na kushuka kwa thamani ya sarafu hizo.

    Leo katika Makala ya Gurudumu la Uchumi, tunajiuliza: Je, sarafu za kidijitali ‘cryptocurrency’ ni uwekezaji wa kweli, au ni uwekezaji wenye hatari kubwa ambao watu wanapaswa kuuchukulia kwa tahadhari?

    15 July 2026, 3:30 pm
  • 9 minutes 56 seconds
    Kodi na Maendeleo: Je, tunapata thamani ya kodi tunazolipa?

    Katika makala ya Gurudumu la Uchumi hivi leo, tunajadili nafasi ya kodi katika maendeleo ya uchumi, umuhimu wa kulipa kodi, na jinsi serikali na wananchi wanavyoweza kushirikiana kujenga uchumi imara na wenye manufaa kwa wote.

    8 July 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 4 seconds
    Je, kukopa kunasaidia ukuaji wa uchumi au kunaleta hatari za siku zijazo?

    Msikilizaji nchi nyingi za Afrika Mashariki zimeendelea kukopa ili kufadhili maendeleo, na huku wadau wengine wakisema mikopo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi, Wengine wanaonya kuwa madeni yanapoongezeka kupita kiasi, serikali hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa madeni hayo badala ya kuboresha huduma muhimu kama vile afya, elimu na ajira.

    Katika Makala ya Gurumu la Uchumi hivi leo, tunauliza: Je, deni la taifa ni daraja la maendeleo au ni mzigo unaoweza kuathiri uchumi wa Afrika?

    24 June 2026, 3:30 pm
  • 10 minutes 3 seconds
    Kutoka taslimu hadi kidijitali: Namna simu zinavyobadili mfumo wa malipo Afrika

    Ufanyaji biashara na utumaji wa fedha kwa njia ya simu za kiganjani barani Afrika unakua kwa kasi, pochi za simu zimerekodi takriban asilimia 19 ya uingiaji wa pesa kwenye eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara, huku wastani wa gharama ya utumaji pesa ukishuka hadi karibu asilimia 3.54 hii ni kwa mujibu wa benki ya dunia.

    Kwanye Makala ya Gurudumu la uchumi wiki hii, tunaangazia matumizi ya telknolojia za malipo ya mtandaoni hasa kupitia simu, jina langu ni Emmanuel Makundi, Karibu.

    10 June 2026, 4:13 pm
  • More Episodes? Get the App